Loading...

Joachim Low kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane?

Kipigo kutoka kwa mahasimu wao Barcelona kimemweka kwenye kiti cha moto kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane baada ya uongozi wa klabu hiyo kutofurahishwa na kipigo hicho.

Imeripotiwa kuwa Real Madrid kupitia Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez imepanga kumtimua kazi Zidane iwapo tu kama atashindwa kushinda angalau kombe moja kati ya kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) au kombe la ligi kuu ya nchi hiyo (LaLiga).

Nafasi ya Zidane imetajwa kuchukuliwa na kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low ambaye inaelezwa kuwa ndiye mbadala wa Zinade ambaye anapendekezwa na Perez.

Makocha wengine ambao majina yao yanatajwa kuchukua nafasi ya Zidane ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente Del Bosque na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Jupp Heynckes.

Ikumbukwe kuwa Zidane alichukua nafasi ya ukocha wa Real Madrid kutoka kwa Carlo Ancelotti mwaka jana na mafanikio aliyoyapata ni pamoja na kuiwezesha klabu hiyo kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2016.
Joachim Low kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane? Joachim Low kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane? Reviewed by Zero Degree on 4/25/2017 04:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.