Loading...

Rais Magufuli awaomba Watanzania wamuunge mkono

Rais John Magufuli akionesha kabrasha lenye Taarifa za Uhakiki wa Vyeti kwa Watumishi wa Umma baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (kulia) katika hafla iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Sherehe za Kutimiza Miaka Kumi ya Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mjini Dodoma jana. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
RAIS John Magufuli amesema anaitengeneza dawa ya kampuni za simu ambazo zimekuwa hazipeleki fedha serikalini, licha ya kufanya miamala mingi. Alitoa kauli hiyo jana wakati akipokea taarifa ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma na uzinduzi wa sherehe za miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Alisema kampuni za simu zimekuwa zikifanya miamala mingi lakini fedha hazifiki serikalini. “Dawa yao tunaitengeneza, baada ya muda mfupi jibu litapatikana, wanafanya transactions (miamala) nyingi lakini fedha haifiki serikalini,” alisema.

Aidha Rais Magufuli amewataka wananchi kila mtu kwa itikadi yake kumuunga mkono ili aweze kufanya kitu ambacho kitawaletea maendeleo Watanzania.

Alisema maendeleo hayana chama na tangu ameingia madarakani amechukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuwezesha taifa kusonga mbele.

“Bahati mbaya nchi hii imeshikwa na mtu ambaye si mwanasiasa, nilipokuwa chuoni nilikuwa nachukia sana wanasiasa, ni waongo,” alisema huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Baada ya Rais Magufuli kupokea taarifa yenye majina ya watu walioghushi vyeti, aliomba mkasi na kukata kamba ya kasha lenye vitabu vya orodha hiyo huku akimtangaza Abdallah Chanya kutoka Mkoa wa Simiyu kuwa ni miongoni mwa watumishi wa umma walioghushi vyeti.

“Huyu ni miongoni mwao,” alisema Rais Magufuli na kubainisha kuwa atakwenda kupitia vitabu hivyo vyote. Aidha kuhusu kuendelea kujengwa kwa miradi ya maendeleo; alisema zitajengwa barabara za kisasa (ring roads) kutoka Chamwino hadi Nala. 

“Tutaanzisha mpango wa reli, uwezo tunao nchi hii ni tajiri tunaweza, Watanzania waipe serikali nafasi wasiikwamishe ili tufikie malengo,” alisema.
Rais Magufuli awaomba Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli awaomba Watanzania wamuunge mkono Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 01:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.