Simba yatinga fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam
Klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga goli moja kwa bila klabu ya Azam FC.
Simba imefuzu kucheza fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa goli lililofungwa na Mohammed Ibrahim katika dakika ya 48 ya mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Baada ya kufuzu fainali, Simba sasa itapambana hatua ya fainali na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Mbao FC na Yanga, mchezo ambao utapigwa kesho jijini Mwanza.
Baada ya kufuzu fainali, Simba sasa itapambana hatua ya fainali na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Mbao FC na Yanga, mchezo ambao utapigwa kesho jijini Mwanza.
Akizungumza kuhusu mchezo huo, nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema, “Kwetu ushindi umetupa furaha sana, kiu ya Wanasimba ni kushiriki michuano ya kimataifa, mpira ulikua mzuri tunamshukuru Mwenyezi Mungu hakuna majeruhi.”
Kwa upande wa Azam FC, nahodha wa wanalambalamba hao, John Bocco amesema,“Tumejaribu kadri ya uwezo wetu, tumejaribu kutengeneza nafasi kipindi cha kwanza na kipindi cha pili lakini nahisi kadi nyekundu ya kipindi cha kwanza ilitudhooofisha.”
Simba yatinga fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam
Reviewed by Zero Degree
on
4/29/2017 11:42:00 PM
Rating: