Wagonjwa wa Malaria nchini kufanyiwa vipimo bure
Kipimo cha MRDT. |
Imesema kwamba kutokana na malalamiko kuwa wapo wanaowatoza fedha wagonjwa wanaokwenda kupina kipimo hicho wakati ni bure, hivyo itawachukuliwa hatua kali.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mjini Dodoma jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema baadhi ya vituo vya umma vimekuwa na tabia ya kutoza wagonjwa vipimo vya malaria na dawa mseto wakati si halali.
“Napenda kusisitiza vituo vya umma vinavyotumia vipimo vya MRDT kwa wagonjwa wa malaria, vipimo hivyo ni bure na pia mgonjwa asilipishwe fedha kwa dawa za mseto ama yule anayelazwa kuchomwa sindano ya ugonjwa huo,” alisisitiza Waziri Ummy.
Ummy aliwataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kuhakikisha kuanzia sasa wanawafuatilia wahudumu wote watakaokiuka agizo hilo kwani watachukuliwa hatua mara moja.
Aidha, aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuwaumbua wahudumu wa afya ambao watawalipisha fedha pale watakapopima maambukizi ya malaria kupitia kipimo cha MRDT ama watakapopewa aluu.
Waziri Ummy pia alizionya maabara binafsi ambazo zimekuwa zikifanya kazi zake kwa kuangalia zaidi fedha badala ya maisha ya mtu kama kuwaambia wana maambukizi ya malaria wakati hawana.
“Maabara nyingi binafsi zimelalamikiwa, mgonjwa anapohisi kuumwa malaria akienda kupima anaambiwa ana wadudu wa malaria wakati si kweli…sasa tumeanzisha mkakati maalum kwa kushirikiana na wizara kuzitafuta maabara hizo,” alisema.
Akizungumzia maadhimisho hayo nchini, Ummy alisema takwimu kutoka vituo vya kutolea huduma za afya zinaonyesha wastani wa watu milioni 12 huripotiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kwa mwaka.
Alisema takwimu za viashiria vya malaria kutokana na tafiti zilizofanyika katika kaya zinaonyesha maambukizi kwa mwaka 2008 ni asilimia 18, 2012 (10) na 2015 ni (14.8).
“Utafiti wa 2015/16 unaonyesha mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma kuwapo na viwango vikubwa vya maambukizi ya malaria, huku makundi yaliyoathiriwa zaidi ni wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano,” alisema.
Hata hivyo, alisema tiba sahihi ya malaria imeendelea kutolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuhakikisha vipimo vya kutambua uwapo wa vimelea vyake kwa kutumia hadubini au MRDT.
Alisema serikali inaendelea kuhakikisha wataalamu wanajengewa uwezo kwa kuwapatia mafunzo ili kufanya kazi kwa ufanisi na weledi, hivyo ongezeko la upimaji ufikie asilimia 90 katika vituo hivyo, zaidi ya lengo la Wizara iliyojiwekea la asilimia 80.
Kuhusu changamoto, Waziri Ummy alisema jamii haitumii ipasavyo vyandarua vinavyotolewa na serikali kwa ajili ya kujikinga ugonjwa huo, huku wengine wakitumia kufugia na shughuli za uvuvi.

Reviewed by Zero Degree
on
4/26/2017 01:08:00 PM
Rating: