Conte amemtaja mchezaji anayefaa kumrithi Terry kwenye nafasi ya Unahodha msimu ujao
Ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu imefika mwisho na wengi wanajaribu kujiuliza ni nani atakaye kuwa Nahodha wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/17 kwa msimu ujao!
Kufuatia kuondoka kwa nahodha wa sasa, John Terry, mashabiki wanahamu ya kusikia ni nani atayekuwa mrithi wake kwa msimu ujao ambapo Chelsea pia itashiriki Ligi ya Mabingwa (UEFA).
Garry Cahill amekua akibeba jukumu la Unahodha wakati Terry alipokua katika Benchi, hata hivyo, Garry Cahill ndiye atakayekuwa Nahodha mpya wa Chelsea msimu ujao?
Hata hivyo, mwamuzi wa mwisho katika hilo ni meneja wa chelsea, Antonio Conte ambaye aliulizwa juu ya jambo hilo na waandishi wa habari.
"Garry amekuwa Nahodha msaidizi msimu huu. Ametekeleza majukumu ya unahodha wakati ambapo John Terry hakucheza", alisema Conte.
“Kwa hakika, Garry ana sifa kubwa ya kuwa Nahodha, lakini kwa sasa ni vema kufikiria zaidi kuhusu kumalizia msimu huu.
“kuanza kufikiria kuhusu msimu ujao ni hatari sana kwa sababu bado tuna malengo mengine tunahitaji kuyafikia kabla ya msimu kuisha.”
Conte amemtaja mchezaji anayefaa kumrithi Terry kwenye nafasi ya Unahodha msimu ujao
Reviewed by Zero Degree
on
5/20/2017 08:03:00 PM
Rating: