Kauli ya Kaburu kuelekea fainali ya FA kati ya Simba na Mbao FC
Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe (kulia) |
Simba itashuka dimbani Mei 27 kuikabili Mbao FC katika pambano la Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (FA) litakalopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.
Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema anaamini huu ni wakati wa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa kitu kimoja ili timu yao iweze kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa hapo mwakani.

“Mimi sina tofauti na wazee wa Simba, nawaheshimu sana, lakini utaratibu waliotumia kutoa malalamiko yao si sahihi, Simba ina kamati zake mbali mbali wangeweza kupeleka malalamiko yao huko tukayamaliza ndani kwa ndani ili kuepusha migogoro hasa wakati huu.
“Sasa hivi tunatakiwa tushikamane tuweke tofauti zetu pembeni, baada ya mchezo wetu na Mbao FC turudi ndani tusemane, tukosoane na mwisho wa siku tutafikia mwafaka kwa ajili ya maendeleo ya Simba,” alisema Kaburu.
Kauli ya Kaburu kuelekea fainali ya FA kati ya Simba na Mbao FC
Reviewed by Zero Degree
on
5/20/2017 01:05:00 PM
Rating: