Mkaa kwa matumizi ya ndani ruksa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema agizo lake la katazo la biashara ya mkaa linalenga biashara ya kimataifa na si mkaa kwa matumizi ya ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe |
Waziri Maghembe alitoa kauli hiyo jana Bungeni mjini Dodoma, na kutoa agizo kwa maofisa maliasili na misitu ambao wanashikilia baiskeli na pikipiki za watu waliokamatwa wakiwa na mkaa kuziachia mara moja.
Pamoja na hilo Prof. Maghembe ameagiza minada ya ng'ombe waliokamatwa kwenye hifadhi za taifa usimame mara moja hadi atakapotoa maelekezo.
"Kilichokatazwa ni wale wanaokata mkaa kutoka msituni na kupeleka nje ya nchi, sisi hatuwezi kukubali misitu yetu kukatwa na kupeleka mkaa Kenya na nchi nyingine za jirani tunataka mkaa ukikatwa utumike Tanzania." alisema Maghembe.
Pamoja na hilo Prof. Maghembe ameagiza minada ya ng'ombe waliokamatwa kwenye hifadhi za taifa usimame mara moja hadi atakapotoa maelekezo.
Source: Nipashe
Mkaa kwa matumizi ya ndani ruksa
Reviewed by Zero Degree
on
5/25/2017 11:36:00 PM
Rating: