Loading...

Sumatra mkoani Mbeya yasitisha utoaji wa leseni za 'Vipanya'

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni za usafirishaji kwa wamiliki na wasafirishaji kwa kutumia gari ndogo aina ya Hiace maarufu ‘Vipanya’ zinazofanya safari zake ndani ya Jiji la Mbeya (daladala) na badala yake inatoa leseni kwa usafiri wa mabasi makubwa aina ya Coaster.

Meneja wa Sumatra Kanda za Juu Kusini, Denis Daudi alisema lengo la kuziondoa Hiace ni kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na kuboresha zaidi huduma ya usafiri wa daladala kama ilivyo kwa majiji mengi nchini.

Amesema tayari wamiliki wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria ndani ya jiji hilo walishatangaziwa hivyo Sumatra haitoa leseni nyingine ya kuendelea kutoa kibali baada muda wake kuamaliza na badala yake leseni atakayopewa mmiliki ni ya kufanyia biashara hiyo nje ya jiji.

Tunachokifanya kwa sasa vipanya vyote vilivyopo barabarani hatuviondoi kwa vile leseni yao bado inaendelea kufanya kazi, ila itakoma tu pale itakapoisha na kutakiwa kukata leseni nyingine, hapo mmiliki atapewa leseni ya kuruhusiwa kufanya biashara hiyo nje ya jiji. Na sasa tunatoa leseni kwa mabasi makubwa aina ya Coaster na tunashukuru na abiria wanaiunga mkono Sumatra katika mabadiliko haya,” amesema Daudi.
Sumatra mkoani Mbeya yasitisha utoaji wa leseni za 'Vipanya' Sumatra mkoani Mbeya yasitisha utoaji wa leseni za 'Vipanya' Reviewed by Zero Degree on 5/20/2017 05:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.