Halimashuri zote nchini zaagizwa kutoa kadi za matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza
Serikali imesema inakamilisha taratibu za kutunga sheria ya bima ya afya kwa wote, itakayo bana halmashauri nchini kulipia kadi za bima ya mfuko wa jamii kwa makundi yenye msamaha ikiwemo wazee wasiojiweza.
Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akiziagiza halmashauri zote nchini kutoa kadi za matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza ili kuwawezesha kupata huduma ya matibabu bila ya usumbufu.
Amesema uanzishwaji wa bima ya afya ya lazima kwa kila mtu itasaidia kuboresha huduma za afya kwani kila mwananchi atachangia gharama za huduma ya afya.
“Wakurugenzi wa halmashauri waendelee kutoa kadi za huduma ya afya ili wazee wasiojiweza waendelee kupewa matibabu. Mikakati tunayo ya kutosha kuhakikisha tunaboresha huduma za afya nchini tuna mkakati wa miaka mine, ingawa hatuna uwezo kiuchumi wa kutekeleza mpango huu kwa asilimia mia lakini tunajitahidi,” amesema.
Amesema uanzishwaji wa bima ya afya ya lazima kwa kila mtu itasaidia kuboresha huduma za afya kwani kila mwananchi atachangia gharama za huduma ya afya.
“Serikali ilishaliona hilo siku nyingi, tukitunga sheria ya bima ya afya kwa wote ya lazima tutatengeneza utaratibu hapa Bungeni kwamba wazee na makundi yote wanayopewa msamaha wa kupata huduma za afya bure wakatiwe kadi za bima ya afya na serikali na utaratibu wa kupata pesa utatengenezwa katika sheria hiyo,” amesema.
Halimashuri zote nchini zaagizwa kutoa kadi za matibabu ya bure kwa wazee wasiojiweza
Reviewed by Zero Degree
on
6/06/2017 07:26:00 PM
Rating: