Homa yaua nguruwe zaidi ya 250 Dodoma, Manispaa yaingilia kati biashara ya nguruwe
Manispaa ya Dodoma imeweka zuio la muda kwa mifugo aina ya nguruwe baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa ugonjwa huo hauna madhara kwa binadamu hivyo wafanyabiashara wanaochinja wanyama jamii ya nguruwe wanapaswa kupata kibali tu ili kuwepo na usimamizi.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari kwa niaba ya Ofisa mifugo wa Manispaa ya Dodoma Ramadhan Juma, leo (Jumamosi) alisema hadi jana jumla ya nguruwe 285 walikuwa wamekufa katika Kata mbili za Ipagara na Miyuji.
Mnyama yoyote wa jamii ya nguruwe (nguruwe, ngiri pori, au nguruwe wa kufugwa) haruhusiwi kutoka au kuingia katika wilaya ya Dodoma bila ya kibali maalumu cha maandishi kutoka kwa ofisa Mifugo wa Manispaa ya Dodoma.
Jana mfanyabiashara wa nyama ya nguruwe kutoka Ipagara Asheri Lyamba amesema ugonjwa huo sio wa karibuni kwani imechukua muda tangu waanze kuziona dalili za kuugua kwa nguruwe.
Lyamba amesema nguruwe huonekana wakitetemeka na kuonza kupoteza hamu ya kula na mwisho wanadhoofu kabla ya kufa au wafugaji kuwauza kwa bei ya chini zaidi.

“Ni kweli taarifa inayosambaa ni ya kwangu, nilituma baada ya kupewa kibali cha kufanya hivyo, hadi leo (jana) nguruwe waliokufa Kata ya Miyuji ni 200 na katika Kata ya Ipagara wamekufa nguruwe 85,” amesema Juma.
Mnyama yoyote wa jamii ya nguruwe (nguruwe, ngiri pori, au nguruwe wa kufugwa) haruhusiwi kutoka au kuingia katika wilaya ya Dodoma bila ya kibali maalumu cha maandishi kutoka kwa ofisa Mifugo wa Manispaa ya Dodoma.
Jana mfanyabiashara wa nyama ya nguruwe kutoka Ipagara Asheri Lyamba amesema ugonjwa huo sio wa karibuni kwani imechukua muda tangu waanze kuziona dalili za kuugua kwa nguruwe.
Lyamba amesema nguruwe huonekana wakitetemeka na kuonza kupoteza hamu ya kula na mwisho wanadhoofu kabla ya kufa au wafugaji kuwauza kwa bei ya chini zaidi.
Homa yaua nguruwe zaidi ya 250 Dodoma, Manispaa yaingilia kati biashara ya nguruwe
Reviewed by Zero Degree
on
6/11/2017 09:34:00 AM
Rating: