Loading...

Wakandarasi watakaojenga miundombinu chini ya kiwango kuchukuliwa hatua kali


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr,John Pombe Magufuli amesema wakandarasi ambao wameingia mkataba na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo barabara,shule na vituo vya mabasi watachukuliwa hatua kali za kisheria endapo watajenga chini ya kiwango au kushindwa kumaliza kazi yake kwa muda.

Mheshimiwa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Korogwe katika uzindisu wa kituo kikuu cha mabasi kilichogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4 chini ya mkopo wa Benki ya Dunia ambapo amesifu kazi nzuri iliyofanywa na mkandarasi NAMIS.

Aidha ameonya baadhi ya watu ambao ni wanaotumia vibaya fedha za serikali katika halmashauri na kueleza kuwa bado sheria za haraka zichukuliwe dhidi ya watu ambao wanashindwa kuleta maendeleo kwa wananchi an badala yake wanatumia vibaya madaraka yao hatua aliyoielezea kuwa watahakikisha kuwa wanakamatwa na kufuguliwa mashtaka.

Awali Naibu Waziri nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo amesema kituo hicho cha mabasi kimejengwa kwa muda muafaka na ni miongoni mwa miradi inayosimamiwa na wizara yake ambayo imeleta sifa kwa nchi kwa ujenzi wenye vigezo vya ushindani.
Wakandarasi watakaojenga miundombinu chini ya kiwango kuchukuliwa hatua kali Wakandarasi watakaojenga miundombinu chini ya kiwango kuchukuliwa hatua kali Reviewed by Zero Degree on 8/08/2017 01:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.