Andrea Pirlo ataja tarehe ya kustaafu Soka
Licha ya kwamba kasi yake imepungua kidogo, Andrea Pirlo mwenye umri wa miaka 38, bado ana shauku kubwa katika mchezo wa soka na pamoja na hayo yote anabakia kuwa mkongwe wa pekee.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2006 atastaafu mwisho wa mwaka huu na ameitumikia City kwa takribani miaka mitatu lakini ameonekana mara 15 tu uwanjani katika mechi 32 za msimu uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la 'Gazetta Dello Sport' ltalia, Pirlo alipoulizwa anamipango gani mkataba wake utakapomalizika, alisema: “Unagundua kuwa muda umeisha.
“Kila siku unapopata matatizo katika mwili, huwezi kufanya mazoezi kama upendavyo kwa sababu tayari mwili wako umechoka.
“Si kwamba unaweza kuendelea hadi miaka ya 50. Nitafanya jambo jingine sahihi.”
Andrea Pirlo ataja tarehe ya kustaafu Soka
Reviewed by Zero Degree
on
10/08/2017 04:01:00 PM
Rating:
![Andrea Pirlo ataja tarehe ya kustaafu Soka](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpbJa9PsNKjbK8pylrkcllcsp2thyphenhyphenAjrvDtezKvdFdyvJsK2vZi_K0vuqBU-_2VKGvqUQltRo5ahUmBN77WYj_rFVsr5eQY63WDHbrIZwj1OIoyche9rSBohmKtY2bKBf_hyn5sgc5NFs1/s72-c/Andrea-Pirlo.jpg)