Bilioni 72 zatolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru |
Kiasi cha Sh72.2 bilioni mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 21,677 kati ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh 108.8 bilioni kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 8,323 watapangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 36.6 bilioni katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.
Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.
“Idadi ya wanafunzi 21,677 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018,” imesema taarifa hiyo
Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.
Bilioni 72 zatolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
Reviewed by Zero Degree
on
10/26/2017 04:38:00 PM
Rating: