Cristiano Ronaldo atangazwa kuwa Mchezaji Bora kwa mara nyingine
Nyota huyo wa Real Madrid ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo akiwapiku wachezaji wenzake, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Ronaldo de Lima na Diego Maradona ndio waliomkabidhi tuzo hiyo Cristiano Ronaldo.
Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Nawashukuru wale wote walionipigia kura."
“Nashukuru pia kwa uwepo wa Messi na Neymar.
“Nawashukuru wachezaji wenzangu, kocha na rais wa klabu ya Real Madrid kwa kuchangia sehemu kubwa ya mafanikio yangu mwaka huu.
“Tuko Uingereza kwa mara ya kwanza, hakika nina furaha, ni wakati wa mzuri kwangu mimi.
“FIFA wanatoa nafasi kwa mashabiki nami ninatambua ya kuwa nina mashabiki wengi duniani kote.
“Najisikia vizuri kubwa kuzungukwa na wachezaji wakubwa kama Maradona na wengineo."
Wengine waliopata tuzo za FIFA ni;
- Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane -Tuzo ya Kocha Bora
- Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud - Tuzo ya Goli Bora la mwaka
- Mlinda mlanbo wa Juventus, Gianluigi Buffon - Tuzo ya Golikipa Bora
- Nyota wa Uholanzi, Lieke Martens - Tuzo ya Mchezaji Bora kwa wanawake
Cristiano Ronaldo atangazwa kuwa Mchezaji Bora kwa mara nyingine
Reviewed by Zero Degree
on
10/24/2017 12:31:00 AM
Rating: