Hii ndio ''First Eleven'' ya pekee iliyopangwa na Ronaldo de Lima
Hata hivyo, yeye kama yeye (Ronaldo) amemuweka pembeni Mreno (C. Ronaldo) huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon D'Or mara nne kwenye kikosi chake bora cha miaka yote.
Ronaldo, kama wajina wake C. Ronaldo ambaye pia aliichezea Real Madrid kama mshambuliaji, yeye binafsi amempa nafasi Lionel Messi kwenye kikosi chake kama kiungo.
Katika maisha ya soka, Ronaldo, alifanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara mbili.
![]() |
Ronaldo amewachagua wachezaji wanne wa Brazili, wanne wa Italia, wawili wa Argentina na Mfaransa mmoja katika kikosi chake |
Ronaldo anawachagua wenzake toka Brazil, Cafu na mtaalamu wa mipira ya adhabu, Roberto Carlos katika nafasi ya beki wa pembeni.
Wakati Cristiano Ronaldo anaachwa nje, meneja wake wa Real Madrid, Zinedine Zidane yuko ndani ya kikosi hicho katika nafasi ya kiungo pamoja na Andrea Pirlo.
Uhasimu kati ya Brazil na Argentina umewekwa pembeni katika nafasi ya winga, baada ya Diego Maradona na Lionel Messi kupewa kibarua cha kuwatengenezea mipira Ronaldo na Pele.

Hii ndio ''First Eleven'' ya pekee iliyopangwa na Ronaldo de Lima
Reviewed by Zero Degree
on
10/08/2017 02:21:00 AM
Rating:
