Wachezaji waliopigiwa kura na Eden Hazard kwenye tuzo za FIFA
Ronaldo alipata ushindi huo kwa asilimia 43%, Lionel Messi alishika nafasi ya pili kwa kuwa na asilimia 19% na watatu akiwa Neymar aliyepata asilimia 6% ya kura zilizopigwa.
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard alimpa nafasi ya kwanza mchezaji mwenzake, N’Golo Kante huku nafasi ya pili akimpa Cristiano Ronaldo na ya tatu akimpa kiungo wa Real Madrid, Lukas Modric.

Nahodha huyo wa Ubelgiji hakuwa mchezaji pekee aliyempa nafasi ya kwanza N'Golo Kante, bali walikuwepo na wengine ambao pia walimpigia kura N'Golo Kante kama vile, Lesly St Fleur (Nahodha wa Bahamas) na Euclid Bertrand (nahodha wa Dominica).
Wakati huo huo, nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson alimpa nafasi ya kwanza Cristiano Ronaldo, ya pili akampa Lionel Messi na ya tatu kwa Luis Suarez.
Wachezaji waliopigiwa kura na Eden Hazard kwenye tuzo za FIFA
Reviewed by Zero Degree
on
10/24/2017 03:14:00 PM
Rating: