Kauli ya Makelele kuhusu mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 alifanikiwa kuyazoea mazingira mapya haraka, akifanikiwa kuifungia Chelsea magoli 7 ikiwemo na 'hat-trick' aliyopata wakati Chelsea ikicheza dhidi ya Stoke City mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Makelele alimtaja morata kwama mchezaji mzuri, mwenye nguvu, mshindani na wa kimataifa.
‘‘Ni mchezaji mzuri. Ametokea katika timu bora duniani, Real Madrid, alifunga magoli ya kutosha pale. Alienda Juventus, pia akafunga magoli ya kutosha kulingana na nafasi aliyopata. Bila shaka atafunga magoli ya kutosha akiwa Chelsea pia.’’
Morata alitolewa nje kufuatia majeraha aliyopata kwenye paja wakati Chelsea ikichapwa goli 1-0 dhidi ya Manchester City lakini atafurahia kucheza chini ya uongozi wa Conte, alisema Makelele.
‘‘Ligi Kuu ya Uingereza ni ngumu, tena ni ngumu sana,’’ kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa aliongeza. ‘‘Nafikiri anaielewa Ligi Kuu. Anaelewa pia ni wapi aliko kwa sasa, kinachotakiwa apewe mipira ya kutosha. Nafikiri atafurahia kuwa na Chelsea.’’
Chelsea wanatarajiwa kutua dimbani kucheza dhidi ya Crystal Palace tarehe 14 Octoba kufuatia kumalizika kwa mechi za kimataifa lakini Morata yuko hatarini kuukosa mchezo huo.
Kauli ya Makelele kuhusu mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata
Reviewed by Zero Degree
on
10/07/2017 09:05:00 AM
Rating:
