Loading...

Kenyatta atangazwa kuwa mshindi wa urais Kenya


Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Rais mteule wa taifa hilo na William Ruto kuwa naibu wake baada ya kushinda uchaguzi wa marudio ambao ulifanyika alhamisi ya Oktoba 26.

Kenyatta ameibuka mshindi baada ya kupata kura 7,483,895 sawa na asilimia 98.27% ya kura zote zilizopigwa na Raila Odinga ambaye aliogomea uchaguzi huo akipata kura 73,228.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati amesema uchaguzi wa marudio ulikuwa huru na wa haki kwa pande zote za vyama ambavyo vilishiriki uchaguzi huo ambao ulisusiwa na Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA).

Chebukati amesema uchaguzi ulifanyika katika kaunti 47 na majimbo 25 yaliyopo Nyanza wananchi wakishindwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali zikiwepo za kiusalama ambapo awali Makamu Mwenyekiti wa IEBC, Consolata Nkatha alisema hata kama uchaguzi ungefanyika katika eneo hilo usingeweza kubadili matokeo ya uchaguzi.

Uchaguzi huo wa marudio umefanyika kufuati mahakama kuu ya Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8 ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi na hivyo kuagiza uchaguzi mwingine ufanyike.
Kenyatta atangazwa kuwa mshindi wa urais Kenya Kenyatta atangazwa kuwa mshindi wa urais Kenya Reviewed by Zero Degree on 10/31/2017 12:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.