Loading...

Kylian Mbappe atwaa tuzo ya 'Golden Boy'


Nyota wa PSG, Kylian Mbappe ameshinda tuzo ya mchezaji bora  "Golden Boy" mbele ya Gabriel Jesus na Ousmane Dembele, ambao walikuwa kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji watatu waliokuwa wanawania tuzo hiyo.

Tuzo hiyo hutolewa kwa mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 21 barani Ulaya na mshindi hupatikana baada ya kura kupigwa na waandishi wa habari ndani ya bara hilo.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 aling'ara akiwa na Monaco msimu uliopita na ameshafunga magoli 4 na kutoa 'assist' 4 katika mechi 11 akiwa Paris Saint-Germain msimu huu kwa mkopo.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa ameibuka na ushindi huo kwa kupata kura 291 akimpiku Dembele aliyekaa nafasi ya pili kwa kupata kura 149.

Wayne Rooney (mwaka 2004) na Raheem Sterling (mwaka 2014) walifanikiwa kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa mchezaji ambaye alionyesha kiwango cha hali ya juu kwa msimu unaokua umemalizika awali.
Kylian Mbappe atwaa tuzo ya 'Golden Boy' Kylian Mbappe atwaa tuzo ya 'Golden Boy' Reviewed by Zero Degree on 10/23/2017 06:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.