Loading...

Mugabe ateuliwa kuwa balozi wa WHO


Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika.

Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O., Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus, alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.

Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara , na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu.

Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.
Mugabe ateuliwa kuwa balozi wa WHO Mugabe ateuliwa kuwa balozi wa WHO Reviewed by Zero Degree on 10/22/2017 01:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.