Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Octoba, 2017


Real Madrid wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, msimu ujao.

Newcastle wanataka kumrejesha mchezaji wa kiungo cha kati ya wa Ufaransa Hatem Ben Arfa,30, kutoka Paris St-Germain. 

(Chanzo: Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anammezea mate mchezaji wa Benfica Alex Grimaldo, 22. 


Mshambuliaji Basel Dimitri Berlin, 20, amethibitisha kuwa alikataa ombi la kuhamia Manchester United mwaka 2014. 

(Chanzo: Metro)

Manchester United wanajiandaa kumpa kiungo wa klabu ya Real Madrid na Brazil Casemiro, 25, mshahara mnono kumshawishi kuondoka Bernabeu ili aelekee Old Trafford.


Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anaweza kupata pauni miioni 500 kwa msimu ujao ikiwa mwanamke mfanyabiashara raia wa Uingereza Amanda Staveley atafanikiwa kukinunua klabu hiyo. 

(Chanzo: Express)

West Ham wanamtaka meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancin, kuchukua mahala pa Slaven Bilic ikiwa atashindwa kuboresha matokeo mabaya ya klabu hiyo. 


(Chanzo: Mirror)

Barcelona wanajiandaa kumpa mkataba wa maisha mshambuliaji Lionel Messi,30, katika klabu hiyo. 


(Chanzo: ESPN FC)

Manchester United watajaribu kumasajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21, Carlos Soler, kutoka Valencia kwa kiasi cha dola milioni 30. 


(Chanzo: Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/22/2017 05:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.