Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 29 Octoba, 2017

Lionel Messi akiwa na familia yake
Lionel Messi anaweza kuichezea Catalunya endapo FIFA itaitambua kama taifa linalojitegemea.

Everton wameingia katika kinyang'anyiro cha kuwinda saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez.

Eddie Nketiah anatarajia kusaini dili jipya na klabu ya Arsenal, ambapo anategemea ongezekao la zaidi ya asilimia 650% kwenye mshahara wake wa sasa.

Alan Pardew
Aliyekuwa meneja wa klabu za Crystal Palace, Newcastle na Southampton, Alan Pardew amekataa ofa kukinoa kikosi cha Dynamo Kiev.

Nyota wa zamani wa klabu ya Bolton, Ivan Klasnic amefanyiwa upausaji kwa mara ya tatu.(Sun)

Manchester City wamepanga kuachana na mpango wa kutaka kumsajili  mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez mwezi Januari.

Bodi ya klabu ya Liverpool imemuahidi, Jurgen Klopp kufanya usajili wa mchezaji yeyote atayemtaka endapo watamuuza Philippe Coutinho mwezi Januari.

Nyota anayewindwa na Liverpool, Zeca yuko tayari kuvunja mkataba wake na klabu ya Santos ili kufanikisha mipango yake ya kuhamia Uingereza.

Bodi ya Everton ipo kwenye vuguvugu la ndani kwa ndani juu ya uchaguzi wa kocha atakayerithi mikoba ya Koeman, ambapo mmiliki wa klabu anamtaka meneja wa klabu ya Watford, Marco Silva.
Mkufunzi wa muda wa Everton, David Unsworth anasema kwamba hakuna shida yoyote endapo atapewa kibaru cha kudumu kukinoa kikosi hicho. (Mirror)

Meneja wa Brighton, Chris Hughton anasema atalisaidia shirikisho la soka la Uingereza (FA) katika kutafuta suluhisho la sula la Eni Aluko. (Mail)

Riyad Mahrez
Mkufunzi mpya wa Leicester, Claude Puel ana mpango wa kumfanya mshambuliaji wake, Riyad Mahrez kuwa na mapenzi na klabu hiyo kama ilivyokuwa awali. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 29 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 29 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/29/2017 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.