Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 30 Octoba, 2017
Zlatan Ibrahimovic amemtaja Anthony Joshua kama "kipenzi cha watu" kwa sasa lakini anasema kuwa anatakiwa kuendelea kuwa na maisha ya kawaida ndani ya jamii inayomzunguka.
Michail Antonio aliambiwa na Slaven Bilic kwamba aliwaangusha wachezaji wenzake wa Westham katika mchezo wao dhidi ya Crystal Palace uliomalizika kwa sare ya goli 2-2. (Daily Mail)
Arsenal wameambia kuwa hawataweza tena kumsajili nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar.
Wakala wa aliyekuwa golikipa wa Real Madrid, Iker Casillas amesema kwamba, suala la Liverpool kumsajili kipa huyo litabakia kuwa ndoto.
Cristiano Ronaldo anaweza kufungiwa michezo kadhaa kufuatia kitendo alichomfanyia kiungo wa Girona Real Madrid ilipochapwa goli 2-1.
Michael Carrick amekuwa nje ya kikosi cha Manchester United kwenye mechi sita zilizopita baada ya kupatwa na kizunguzungu katika mchezo wake wa kwanza na pekee katika msimu huu dhidi ya Burton. Hali yake imeonekana kuimarika mazoezini.
Arsenal watampa mashambuliaji Eddie Nketiah, 18, mkataba mpya wa miaka mitano ambapo mshahara wake utakuwa kati ya pauni 2,000 hadi 15,000 kwa wiki. (Sun)
Klabu za Aston Villa, West Brom na Leicester ziko kwenye harakati ya kusaka saini ya nahodha wa Manchester United, Michael Carrick.
Arsene Wenger ana imani Arsenal wanaweza kuisimamisha rekodi ya Manchester City ya kucheza bila kupoteza mchezo tangu kuanza kwa msimu.
Kevin De Bruyne anaamini kwamba, ni vigumu kwa Manchester City kumaliza msimu bila kufungwa kama ilivyokuwa kwa Arsenal.
Harry Kane kujumuika pamoja na wenzake kwenye mechi yao dhidi ya Real Madrid, lakini Mauricio Pochettino hana imani kama nyota huyo atakuwa kwenye kiwango chake cha siku zote.
Antonio Conte atilia mkazo suala la kuwajumuiasha kwenye kikosi cha kwanza wachezaji wake walioshinda kombe la dunia chini ya miaka 17.
Aliyekuwa meneja wa Watford, Walter Mazzarri yuko kwenye mikakati ya kuchukua nafasi ya meneja wa Torino.
Klabu za Tottenham, Bournemouth na Southampton ziko kwenye harakati za kusaka saini ya kinda wa Timu ya Taifa ya Uingereza chini ya mika 20, Callum Brittain, ambaye anaicheza the MiltonKeys Dons.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anasema kuwa hana uhakika na kiwango cha Paul Pogba atakaporejea kucheza akitokea majeruhi.(Mirror)
Alan Pardew amefanya mawasiliano na klabu ya Rangers kuhusu kuchukua nafasi ya mkufunzi wa klabu hiyo ambayo iko wazi kwa sasa.
Paris Saint-Germain wanaweza kuingilia kati na kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwezi Januari wakati Manchester City wakitarajiwa kumsubiria nyota hadi wakati wa majira ya joto. (Express)
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amewataka mashabiki kuwapa hamasa wachezaji.
Meneja wa Arsenal anasema kwa mshambuliaji Alexi Sanchez ana mkataba kuifanyia mema Arsenal wakati watacheza na Manchester City siku ya Jumapili. (Telegraph)
Wakati Meneja wa klabu ya Burnley Sean Dyche akihusishwa na kuchukua kazi huko Everton, mlinzi wa klabu hiyo, Stephen Ward amesema kumpoteza itakuwa pigo kubwa.
Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale huenda akakosa mechi dhidi ya klabu yake ya zamani Tottenham katika Champions League siku ya Jumatano.(Times)
Kocha wa klabu ya Sunderland, Simon Grayson hatarini kufutwa kazi endapo timu yake itashindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi dhidi ya Bolton siku ya Jumanne.
Mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney anaweza kuadhibiwa na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kufuatia kitendo cha kumkaba shingoni mchezaji wa Stoke City, Joe Allen Jumamosi iliyopita. (Star)
Paris St-Germain wamemuorodhesha mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, kuwa nambari moja kati ya wachezaji ambao wanalenga kuwasaini msimu ujao. (TF1)
Manchester City wanaamini kuwa wanaweza kumpata mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid, Isco, 25, licha ya yeye kusaini mkataba wa muda mrefu huko Bernabeu. (Don Balon)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 30 Octoba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
10/30/2017 03:31:00 PM
Rating: