Loading...

Ujumbe wa Yondani kwa mashabiki wanaomhofia Emmanuel Okwi


Wakati joto la mechi ya watani linazidi kupanda, beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, amesema kuwa, Jumamosi ijayo atahakikisha anamzuia ipasavyo straika wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi na watu watamsahau.

Jumamosi ijayo, Yanga itapambana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar ambapo mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka wa ndani na nje ya Tanzania.

Okwi ambaye kwa sasa anaongoza kwenye chati ya wafungaji katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, anatarajiwa kufanya makubwa kwenye mchezo huo ikiwemo kuisumbua vilivyo ngome ya ulinzi ya Yanga.


Kutokana na hali hiyo, Yondani amesema: “Katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Stand United sikucheza kwa sababu makocha walikuwa wakihofia pengine ningepewa kadi ya njano ambayo ingesababisha niikose mechi dhidi ya Yanga na wala sikuwa majeruhi.

“Hivyo nipo fiti kukabiliana na Simba na huyo Okwi ambaye wanamsifia kwamba yupo vizuri, nitamkaba na watamsahau,” alisema Yondani ambaye amewahi kucheza na Okwi Yanga.

Hata hivyo, Okwi anakwenda kwenye mchezo huu akiwa na heshima ya kuwafunga Yanga mabao matatu kwa kipindi chote na mechi hizo zote Yondani alikuwa uwanjani.
Ujumbe wa Yondani kwa mashabiki wanaomhofia Emmanuel Okwi Ujumbe wa Yondani kwa mashabiki wanaomhofia Emmanuel Okwi Reviewed by Zero Degree on 10/25/2017 11:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.