Loading...

Conte aeleza sababu za kumtoa Bakayoko nje kwenye mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham


Conte ametetea kiwango cha Tiemoue Bakayoko kwenye mechi yao dhidi ya West Ham jana, mechi iliyomalizika kwa 'The Blues' kuchapwa goli 1-0.

Conte anasema kuwa lengo lake lilikuwa kubadilisha mfumo, kwa kumtoa mchezaji anayecheza kwa mfumo wa kukaba zaidi na kumwingiza mchezaji anayeweza kupenya katika ngome ya wapinzani, ambaye alikuwa ni winga wa klabu hiyo, Pedro Rodriguez.


Hata hivyo, Muitaliano huyo alikuwa na furaha kwa kiwango alichokionyesha Bakayoko katika mchezo huo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, alieleza sababu ya kufanya mabadiliko yale: ‘‘Yalikuwa maamuzi ya kiufundi kwa sababu binafsi nafikiri Bakayoko alikuwa anacheza vizuri, lakini unapokuwa na wachezaji 11 wakicheza nyuma ya mpira na tayari ulishafungwa goli 1-0 ni muhimu kufanya mabadiliko kutafuta ufumbuzi mwingine.’’

‘‘Kwa hili, Pedro anacheza mfumo tofauti na Bakayoko. Ni mzuri kwa kucheza uso kwa uso na mpinzani, ni mchezaji mwenye ufundi zaidi. Kupoteza mchezaji anayezuia haikuwa muhimu sana baada ya kipindi cha kwanza, lakini ilikuwa ni uamuzi wa kiufundi tu. Bakayoko alinifurahisha kwa kiwango chake.’’
Conte aeleza sababu za kumtoa Bakayoko nje kwenye mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham Conte aeleza sababu za kumtoa Bakayoko nje kwenye mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham Reviewed by Zero Degree on 12/10/2017 06:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.