Ninje aeleza kilichosababisha Kili Stars ishindwe kusonga mbele Challenge Cup
Watanzania bara wengi huenda wanataka kujua sababu za timu yao kushindwa kufanya vyema hata katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashiriki na Kati. Kocha wa Kili Stars ametoa sababu za kikosi chake kuburuzwa huko nchini Kenya.
“Nimepata mda mfupi, nimefanya mazoezi na timu mara mbili au mara tatu, mara ya kwanza sikuwa na timu yote, Jumanne nikapata wachezaji, Jumatano tukafanya mazoezi, Alhamisi tumekuja huku kwa hiyo matayarisho hayakuwa mazuri lakini isiwe sababu ya sisi kushindwa. Matayarisho yanaweza yasiwe mazuri lakini mkapambana na mkashinda.”
“Nimejifunza na wenzangu wamejifunza, tutajipanga ili wakati mwingine yasitokee kama haya.”
“Kwa wakati huu tumeshindwa lakini tujitahidi wakati ujao tufanye vizuri. Wachezaji wote wamefanya vizuri, kuna marekebisho ya hapa na pale kwa hiyo mimi klama mwalimu nitakaa nao na kuwaambia ili tukitaka tuendelee kwenye mpira kuna vitu vya kurekebisha ili tuwe kwenye level ya kimataifa.”
“Nataka wachezaji wangu wasifikirie kucheza nyumbani, wafikirie kutoka nje, sasa wamepata bahati mwalimu anafundisha mpira nje ya Tanzania kwa hiyo najua mahitaji ya mpira wa kimataifa sasa nitawaomba wanisikilize, wajifunze badae na wao wapate nafasi ya kutoka nje ya Tanzania.”
Ninje aeleza kilichosababisha Kili Stars ishindwe kusonga mbele Challenge Cup
Reviewed by Zero Degree
on
12/10/2017 05:15:00 PM
Rating: