Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 13 Decemba, 2017

Thomas Lemar
Chelsea ina mpango wa kutoa ofa mwezi Januari kwa ajili ya kumnasa nyota anayewaniwa na Liverpool pamoja na Arsenal kutoka klabu ya Monaco, Thomas Lemar ili kuongeza nguvu katika kikosi cha meneja wao, Antonio Conte.

Manchester City wanakaribia kukamilisha dili la mkataba npya na Gabriel Jesus, utakaomfanya aendelee kusalia na klabu hiyo kwa muda mrefu.

Mohamed Salah anaweza kuwa nyota mwingine wa Liverpool anayetegemewa kuwa nje kwa muda baada ya Jurgen Klopp kueleza kwamba kutolewa kwa nyota huyo kwenye mechi dhidi ya Everton ilikuwa ni tahadhari kufuatia majeraha madogo aliyonayo kwenye paja.

Alan Pardew anatarajiwa kuwa na mkutano na upngozi wa klabu ya West Brom siku ya Ijumaa baada ya kuthibitisha kwamba ana nia ya kumsajili nyota wa Liverpool, Danny Ings.

Claude Puel ameomba rekodi zake katika klabu ya Southampton zilindwe na kusistiza kwamba madhaifu yake hayastahili kupewa nafasi, kuelekea kurejea katika dimba la St Mary. (Telegraph)

Samuel Umtiti 
Jose Mourinho anajiandaa kumtikisa meneja wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde kwa kujaribu kumnasa kiungo tegemezi wa klabu hiyo, Samuel Umtiti ambaye mkataba wake wa sasa unaelekea kumalizika.

James Rodriguez amemshauri Florentino Perez amsajili mchezaji atakayemaliza nguvu klabu ya Barcelona, ambaye ni nyota wa Timu ya Taifa ya Colombia, Yerry Mina.

Nahoda wa Ureno, Cristiano Ronaldo amemtaka rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ahakikishe anafanikiwa kuinasa saini ya Gonçalo Guedes anayeichezea klabu ya Valencia kwa mkopo akiokea PSG (Don Balon)

Chelsea wako mstari wa mbele kufanikisha usajili wa beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro mbele ya Manchester United.

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge atalazimisha kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari kulinda matumaini yake ya kushiriki Kombe la Dunia, huku klabu za Valencia na Real Betis zikiwa na matamanio makubwa ya kumsajili nyota huyo.

West Ham wamejiandaa kumruhusu chipukizi, Reece Oxford ajiunge na klabu ya Borussia Monchengladbach kwa mkataba wa kudumu.

Beki wa klabu ya Manchester City, Danilo anawaniwa na klabu yake ya zamani FC Porto kwa mkopo kuanzia mweji ujao hadi kumalizika kwa msimu huu.

Klabu ya Newcastle inamtaka nyota wa Manchester United, Scott McTominay kwa mkopo mwezi ujao.

Nigeria Vs Algeria
Nigeria itaruhusiwa kushiriki Kombe la Dunia mwakani licha ya kukiuka sheria kwa kucheza mchezaji aliyekosa sifa katika mechi ya kufuzu dhidi ya Algeria iliyomalizika kwa sare na ya goli 1-1 na baadaye kueuzwa na kuwa 3-0 lakini haikuathiri nafasi yao. (Sun)

Ofa ya klabu ya Chelsea ya paundi milioni 22 kumnasa winga wa Bayer Leverkusen, Leon Bailey imekataliwa.

Rafa Benitez amemtaka mmiliki wa klabu ya Newcastle, Mike Ashley amwambie ni kiasi gani cha fedha atakachopewa kwa ajili ya usajili wa wachezaji mwezi Januari kabla ya kumalizika kwa siku ya Ijumaa. (Daily Mail)

Sam Allardyce amefuta sherehe ya chismas katika klabu ya Everton, baada ya kuwaambia wachezaji wake kwamba kiwango chao msimu huu hakiwaruhusu kufanya hivyo. (Guardian)

Ronaldo amesema ana shauku kubwa ya kuungana na Gareth Bale uwanjani, hiyo ikionyesha kwamba anamtaka nyota huyo abaki Bernabeu. (Express)

Mauricio Pochettino atawafanya wachezaji wake watazamie mchezo wao dhidi ya Brighton kwa kuchagua timu yenye nguvu kwa ajili ya mechi ya Jumatano.

Jermain Defoe
Jermain Defoe anatarajiwa kupambana uso kwa uso na Marcus Rashford kwenye dimba la Old Trafford Jumatano, lakini hamchukulii kama mpinzani katika nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia 2018.

Tottenham na Everton zimeingia kwenye orodha ya vilabu vinavyowania saini ya mshambuliaji chipukizi wa klabu ya Hamburg, Jann-Fiete Arp. (Mirror)

Winga wa klabu ya Wolves, Ben Marshall anawaniwa na Cardiff City pamoja na Sheffield Wednesday.

Klabu za Aston Villa, Fulham pamoja na Wolves zote zinamtaka mshambuliaji wa Bournemouth, Lewis Grabban, ambaye kwa sasa anaitumikia Sunderland kwa mkopo. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 13 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 13 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/13/2017 11:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.