Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 11 Decemba, 2017
Thibault Courtois |
Golikipa wa Chelsea, Thibault Courtois amekanusha kudai kulipwa fidia na klabu yake na badala yake amesema anataka mkataba mpya.
Mmiliki wa klabu ya Crystal Palace, Steve Parish alihusika katika mzozo na mashabiki wa timu yake katika dimba la Selhurst Jumamosi.
Antonio Conte ana hofia Chelsea kushindwa kuzikwepa Barcelona na PSG katika droo ya Ligi ya Mabingwa kuepusha msimu wao kuwa mchungu.
Mshambuliaji wa klabu ya Swansea, Oliver McBurnie ni mmoja kati ya nyota wanaowaniwa na Aston Villa.
klabu ya Leeds inatazamia kumsajili nyota wa Sporting Lisbon, Tobias Figueiredo.
Bolton wana matamanio makubwa ya kumrejesha Zac Clough kwa mkopo kutoka klabu ya Nottingham Forest.
Anthony Pilkington |
Cardiff City watamruhusu Anthony Pilkington mwezi Januari. (Mirror)
Jose Mourinho amekuwa na mazungumzo magumu na Marouane Fellaini katika nafasi yake ya mwisho kumfanya asaini mkataba mpya na Manchester United.
Luke Shaw alipwe paundi milioni 5 aondoke Manchester United mwezi Januari.
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema hawezi kumtegemea nahodha wa klabu hiyo, Vincent Kompany.
Josh Eppiah |
Mshambuliaji wa Leicester, Josh Eppiah anawindwa na klabu za Everton, Bournemouth, West Ham na Stoke. (Sun)
Mikel Arteta aliachwa akitokwa na damu baada ya kutokea kwa mzozo kati ya Jose Mourinho na wachezaji wa Manchester City baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu hizo mbili Old Trafford.
Mikel Arteta aliachwa akitokwa na damu baada ya kutokea kwa mzozo kati ya Jose Mourinho na wachezaji wa Manchester City baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu hizo mbili Old Trafford.
Mwenyekiti wa Crystal Palace, Steve Parish ameomba msamaha baada ya kutofautiana na shabiki wa timu hiyo katika mechi yao dhidi ya Bournemouth Jumamosi.
Golikipa wa Stoke City, Jack Butland bado ana ndoto ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia licha ya kuruhusu magoli matano katika mechi yao dhidi ya Tottenham. (Daily Mail)
Alan Pardew amezungumzia mipango yake ya kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji ya West Brom mwezi Januari kufuatia kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Swansea.
Alan Pardew amezungumzia mipango yake ya kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji ya West Brom mwezi Januari kufuatia kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Swansea.
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino anasema kwamba ana hamu kubwa sana ya kupangwa na kigogo yeyote kwenye droo ya Ligi ya Mabingwa Jumatatu.
Roy Hodgson amemtaka Christian Benteke awalipe fidia wachezaji wenzake baada ya kukosa penati na kuifanya klabu yake ikose ushindi dhidi ya klabu ya Bournemouth. (Telegraph)
Pep Guardiola alitetea kitendo chake cha kuunga mkono uhuru wa Catalonia hadharani kufuatia mechi yao dhidi ya Manchester United Jumapili, siku chache zikiwa zimepita baada ya Jose Mourinho kumkosoa na kuhoji kama ni sahihi kwa mameneja kuruhusiwa kutoa matamko ya kisiasa. (Independent)
Beki wa klabu ya West Ham, Jose Fonte amemtuhumu mmiliki wa klabu David Sullivan kuwa kutoa wazo la kusajili beki ilikuwa ni makosa. (Star)
Joe Hart |
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 11 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/11/2017 01:52:00 PM
Rating: