Loading...

Liverpool yapaa hadi nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu


Mohamed Salah alifunga bao la lake la sita mfululizo na kuisadia Liverpool kupanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la ligi kupitia ushindi mzuri uliowafurahisha mashabiki wake dhidi ya West Ham.

Emre Can aliiweka kifua mbele timu hiyo ya mkufunzi Jurgen Klopp kupitia kona-likiwa ni bao la 100 la Liverpool msimu huu baada ya Salah kugonga mwamba.

Salah hatahivyo alifunga bao la pili kupitia mkwaju wa kimo cha nyoka kufuatia kazi nzuri ya Oxlaide Chamberlain kabla ya mshambuliaji mahiri Roberto Firmino kuongeza bao la tatu baada ya makosa ya kipa Adrian.

Shambulizi la chinichini la Michail Antonio liliwapatia West Ham bao la kufutia machozi lakini Mane ambaye alikuwa amegonga mwamba awali akafunga bao la nne.

Matokeo ya mechi nyengine:
  • Leicester 1-1 Stoke
  • Bournemouth 2-2 Newcastle
  • Brighton 4-1 Swansea
  • Burnley 1-1 Southampton
  • West Brom 1-2 Huddersfield
Mechi za Ligi Kuu zitakazocheza kesho:
  • Crystal Palace Vs Tottenham (Saa 3:00 alasiri)
  • Manchester United Vs Chelsea (Saa 5:05 jioni)
Liverpool yapaa hadi nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Liverpool yapaa hadi nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Reviewed by Zero Degree on 2/24/2018 10:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.