Loading...

Mwigizaji nyota wa Bollywood afariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo

Sridevi Kapoor enzi za uhai wake
Mwigizaji nyota wa Bollywood, Sridevi Kapoor amefariki kutokana na mshutuko wa moyo akiwa na miaka 54, familia yake imesema.

Mwigizaji huyo wa filamu, ambaye anafahamika kwa jina la Sridevi alikuwa pamoja na familia yake mjini Dubai kuhudhuria harusi ya mpwa wake.

Ameshiriki kazi za filamu kwa miongo mitano katika ndani ya filamu 300 kama vile Mr India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.

Sridevi Kapoor
Alitajwa kuwa mmoja wa wasanii wachache wa kike waliopata mafanikio makubwa bila ya msaada wa wanaume.

Kutoka akiwa na umri wa miaka minne alikuwa ameshikiri filamu za lugha za Tamil, Telugu, Malayalam, Kannada na Hindi

Umati ulikusanyika nje ya nyumba yake mjini Mumbai wakati habari za kifo chake zilipofichuka. Viongozi na wacheza filamu walielezea kushangazwa na kifo chake.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi aliandika katika mtandao wa twitter juu ya kuhuzunishwa kwake kufuatia tukio hilo, huku rais wa India, Ram Nath Kovind akisema kifo chake kimewavunja moyo mamilioni ya mashabiki.
Mwigizaji nyota wa Bollywood afariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo Mwigizaji nyota wa Bollywood afariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo Reviewed by Zero Degree on 2/25/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.