Loading...

Arsenal wanaweza kufanikiwa kumsajili kiungo huyu kwenye majira ya joto


Arsenal wanatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chao kwenye majira ya joto baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. Wamemaliza ligi katika nafasi ya 6 na watakosa michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Arsene Wenger ataondoka katika klabu hiyo na tayari wanasaka mtu wa kuchukua nafasi yake pamoja na kunguvu nyingine mpya. Safu zilizopewa kipaumbele kikubwa ni sadu ya kiungo na safu ya ulinzi.

Mmoja wa wachezaji ambao wanalengwa na the Gunner ni nyota wa Monaco, Thomas Lemar kuelekea dirisha la usajili. Arsene Wenger alijaribu kumsajili kwenye majira ya jito na ofa ya pauni milioni 88.32 kwa ajili yake lakini mchezaji huyo aliikataa ofa hiyo.

Mfaransa huyo bado ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na vigogo hao wa Ligi Kuu ya Uingereza na wamepata matumaini ya kufanikiwa kumsajili.

Kiungo wa klabu ya Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa, Thomas Lemar
Aliyekuwa mchezaji wa Arsenal anaamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ataondoka Monaco na anaweza kuwa tayari kwa uhamisho huo baada ya Kombe la Dunia. Anadai mchezaji huyo anaweza kuelekea Uingereza kwenye majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa ya bwin, mkongwe huyo alisema: “Thomas Lemar ataondoka Monaco baada ya Kombe la Dunia kwenye majira ya joto.

“Nafikiri anataka kupata changamoto mpya na angependelea kupata uzoefu wa kucheza katika nchi nyingine.

“Bilashaka, Arsenal walikuwa nia ya kumsajili mwaka jana lakini sijui kama bado wana nia yao ya kumnunua kwa sasa ambapo Arsene Wenger hatokuwa meneja. Anaweza akafaa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.”

Lemar amekuwa na wakati mgumu kufikia kiwango chake alichokuwa nacho msimu uliopita lakini amefanikiwa kufunga magoli manee na kutoa 'assist' nane msimu huu. Licha ya kuwa na wakati mgumu, bado ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji Duniani na bado anavivutia vilabu vingi vya Ulaya.
Arsenal wanaweza kufanikiwa kumsajili kiungo huyu kwenye majira ya joto Arsenal wanaweza kufanikiwa kumsajili kiungo huyu kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 5/13/2018 06:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.