Loading...

Barcelona kumuuza nyota huyu kwenda Liverpool kwa mkopo


Vigogo wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Barcelona wameripotiwa kuwa na mpango wa kumuuza chipukizi wa Colombia, Yerry Mina kwa mkopo kwenda Liverpool.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu hiyo akitokea Palmeiras kwa pauni milioni 10 mwezi Januari, baada ya kukidhi kigezo alichokubaliana na klabu yake ya Brail. Lakini amekuwa na wakati mgumu kuonyesha uwezo wa kumvutia meneja wa Barcelona, Erneste Valverde, akifanikiwa kucheza jumla ya mechi tano.

Yerry Mina

Kwa mujibu wa ripoti hizo, hivi karibuni, mwandishi wa habari anayeheshimika sana, Ignacio Miguelez alisema kuwa:

“Kuna mchezaji mmoja, ambaye hatima yake katika klabu hii msimu ujao inajulikana tayari, na huyo ni Yerry Mina.

“Mkolombia huyo atatumikia msimu ujao katika klabu ya Liverpool kwa mkopo.”

Inaeleweka kwamba usajili wa beki huyo haikuwa chaguo la Valverde na meneja huyo anaamini kuwa bado anahitaji muda wa kutosha kuzoea Ligi ya Ulaya.

Safu ya ulinzi ya Liverpool tayari imeonyesha kuimarika tangu mwezi Januari kwa kumsajili Virgil Van Dijk na wekundu hao wako sokoni kusaka mchezaji aliyeimarika aje kucheza pamoja na Mholanzi huyo.
Barcelona kumuuza nyota huyu kwenda Liverpool kwa mkopo Barcelona kumuuza nyota huyu kwenda Liverpool kwa mkopo Reviewed by Zero Degree on 5/16/2018 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.