Loading...

Breaking News: Lulu aachiwa huru, kutumikia kifungo cha nje


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imembadilishia adhabu ya kifungo, Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, ambaye kuanzia sasa atatumikia kifungo cha nje.

Lulu Novemba 13 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake ambaye alikuwa pia mpenzi wake, Steven Charles Kanumba, tukio lililotokea April 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo atatumikia kifungo cha nje.

Amesema pia kwamba, msanii huyo aliachiwa tangu juzi Jumamosi Mei 12, huku akisisitiza kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, ambayo kisheria inaitwa ‘community service'.
Breaking News: Lulu aachiwa huru, kutumikia kifungo cha nje Breaking News: Lulu aachiwa huru, kutumikia kifungo cha nje Reviewed by Zero Degree on 5/14/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.