Loading...

Kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia chatajwa

Nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Jesus (kulia), Neymar (katikati) na Coutinho (kushoto) 
Brazil wamemtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, ambaye bado anauguza jeraha, katika kikosi cha wachezaji 23 ambao wanatarajiwa kuchezea taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Neymar, 26, alifanyiwa upasuaji mwezi Machi na daktari wa timu ya taifa ya Brazil alisema hataweza kucheza kwa miezi mitatu.

Wachezaji wanne wanaochezea Manchester City Ederson, Danilo, Fernandinho na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza, ambao wamo kwenye kikosi hicho.

Wengine ni nyota wa Liverpool Roberto Firmino na winga wa Chelsea Willian.

Beki wa kulia wa PSG Dani Alves atakosa michuano hiyo baada ya kupata jeraha la goti wiki iliyopita.

Brazil wamepangwa Kundi E na Costa Rica, Serbia na Uswizi na watacheza mechi yao ya kwanza Jumapili 17 Juni.

Walinda mlango: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).

Mabeki: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

Viungo wa kati: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).

Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).
Kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia chatajwa Kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia chatajwa Reviewed by Zero Degree on 5/15/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.