Loading...

Liverpool kutumia pauni milioni 60 kumsajili beki huyu

Beki wa kushoto wa klabu ya Benifica, Alex Grimaldo
Liverpool wanatazamia kuushangaza ulimwengu wa soka kwa kutoa karibu pauni milioni 60 kukidhi vigezo vya kuipata saini ya mchezaji chipukizi wa Benifica.

Wekundu hao walifanikiwa kumaliza katika nafasi nne bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza siku ya Jumapili, na sasa wamegeuza macho yao kwenye kuikabili Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Kiev Mei 26.

Licha ya kufanikiwa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa, wameondoka mikono mitupu kwenye michuano ya michuano ya ndani ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu, na hivyo kuongeza nguvu mpya kikosini kwenye majira ya joto inaweza kuwasaidia kuukaribia ubingwa.

Ripoti zimedai kuwa beki wa kushoto wa Benfica, Alex Grimaldo amekuwa miongoni mwa wachezaji ambao Liverpool inalenga kuwasajili, lakini atagharimu pauni milioni 60.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ameonyesha kiwango cha kuvutia msimu huu, akicheza mechi 36 kwenye michuano yote kwa vigogo hao wa Ureno na kufanikiwa kulitangaza jina lake.

Andy Robertson ameitawala nafasi ya beki ya kusho na Alberto Moreno anaweza kuondoka Liverpool na kutoa nafasi kwa Grimaldo kuingia kikosini na kuonyesha uhodari wake.
Liverpool kutumia pauni milioni 60 kumsajili beki huyu Liverpool kutumia pauni milioni 60 kumsajili beki huyu Reviewed by Zero Degree on 5/14/2018 07:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.