Loading...

Ng’ombe wailiokufa wakamatwa wakiingizwa sokoni


Mapema asubuhi ya leo (Jumapili) katika Machinjio ya Tegeta lilikamatwa lori lililopakia ng’ombe waliokufa wakiwa tayari kuingizwa sokoni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Jumanne Muliro amesema kuwa kufariki kwa mifugo ni tukio la kawaida kwani Mifugo inatoka mbali na ikitokea hivyo kuna utaratibu unaotakiwa kufanyika na si kuwaingiza sokoni mifugo hao.

“Malori yanasafiri na mifugo umbali mrefu na mifugo mingine hufariki kutokana na hali hiyo na tayari maafisa mifugo walifika katika eneo la tukio na kuhakikisha wanashughulikia tatizo hilo mapema”. Amesema Kamanda Murilo

Kamanda Muliro ameongeza kuwa Sheria na kanuni zinaeleza endapo likitokea tukio kama hilo nini kifanyike ili kulinda Afya za walaji.
Ng’ombe wailiokufa wakamatwa wakiingizwa sokoni Ng’ombe wailiokufa wakamatwa wakiingizwa sokoni Reviewed by Zero Degree on 5/14/2018 01:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.