Loading...

Nyota Tottenham asaini mkataba mpya wa miaka 6


Beki wa klabu ya Tottenham, Davinson Sánchez amesaini mkataba mpya wa miaka 6 utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2024.

Raia huyo wa Colombia amekuwa na wakati mzuri kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na Spurs baada ya kujiunga na nao akitokea Ajax kwa ada ya pauni milioni 42, ambayo iliweka rekodi katika klabu hiyo kwenye majira ya joto mwaka jana.

Kiwango cha Sánchez kimekuwa cha kuvutia kiasi kwamba Tottenham inafurahia kumruhusu Toby Alderweireld aondoke klabuni baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba kugonga mwamba.

Klabu hiyo ina matumaini ya kufanikiwa kuwashawishi baadhi ya wachezaji wao wa muhimu kubaki hadi msimu ujao, huku ikiwa kwenye maandalizi ya kuhamia kwenye uwanja wao mpya.

Davinson Sánchez 
Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Tottemham kwenye Twitter ilisema: “Tunafurahia kuwatangazia kwamba Davison Sanchez amesaini mkataba mpya na klabu yetu, ambao utaisha mwaka 2024.”
Nyota Tottenham asaini mkataba mpya wa miaka 6 Nyota Tottenham asaini mkataba mpya wa miaka 6 Reviewed by Zero Degree on 5/16/2018 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.