Loading...

Napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri - Mo


Ikiwa ni siku ya tatu tangu kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji 'Mo Dewji', mfanyabiashara huyo ametoa neno la shukrani kwa mwenyezi Mungu na watanzania kwa kumuombea katika kipindi chote alichokuwa mateka.

Kupitia ukurasa wake wa 'twitter' Mo Dewji ameandika kuwa, "Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu".

Mo Dewji ameongeza kuwa, "Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima".

Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima.

Mfanyabishara huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akielekea mazoezini na kuachiwa Alfajiri ya Oktoba 19, ambapo alikutwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana.

Mo Dewji ameandika hivi ukurasa wake wa 'twitter':
Napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri - Mo Napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri - Mo Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.