Loading...

Orodha ya wachezaji 11 wenye umri mkubwa zaidi barani Ulaya

Petr Cech akiwa na Gianluigi Buffon
Kuna watu huwa wanasema maisha huanza unapofikisha miaka 40, na Gianluigi Buffon ni miongoni mwao.


Badala ya kustaafu, golikipa huyo kutoka Italia aliondoka Juventus kwenda Paris Saint-Germain kuendeleza msako wa taji la Ligi ya Mabingwa kabla hajaachana na kazi yake ya kulinda goli.

Ana wachezaji kama nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar na chipukizi mwenye kipaji cha kipekee Kylian Mbappe wa kumsaidia kufanya hivyo na bado anaendelea kuonyesha umahiri wake pale anaposimama golini.

Hata hivyo, Buffon hayuko peke yake. Wapo wakongwe wengi ambao bado wanaendelea kusaka rekodi kwenye soka.

Zero Degree imejaribu kupitia takwimu kutoka tovuti ya WhoScored.com na kuwekea majina ya wachezaji 11 wenye umri miaka 33 na kuendelea kutoka ligi tano kubwa barani Ulaya.

11. Gianluigi Buffon (Paris Saint-Germain)


Akiwa na miaka 40, Buffon alikuwa na ujasiri wa kuondoka Juventus kwenda Paris lakini anaendelea kuonyesha busara zake kwani tayari PSG inaonyesha matumaini ya kutwaa taji tena. Kwa uwezo aliouonyesha kwenye mchezo kati ya PSG na Lyon kabla ya mechi za kimataifa, unaonyesha kwamba bado ni golikipa bora.

10
Petr Cech (Arsenal)


Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa na wakati mgumu kidogo kuendana na mfumo wa Unai Emery na amesharuhusu magoli 9 katika michezo 7, kwa mujibu wa takwimu za WhoScored, alikuwa anafanya vizuri kabla ya kuumia kwenye mechi yao dhidi ya Watford iliyomalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

9. Rune Jarstein (Hertha Berlin)



Kwenye Bundesliga, Hertha wako nafasi ya tano katika ligi yenye mvutano mkubwa na hiyo imechangiwa na rekodi yao nzuri ya ulinzi. Raia huyo wa Norway (Rune, ambaye ni golikipa wao) amesharuhusu mabao 6 pekee msimu huu.

8. Giorgio Chiellini (Juventus)


Wakati Juventus wakijaribu kutwaa taji la Sirie A kwa mara nane mfululizo, Muitaliano huyo bado anaonekana kuwa ni mwamba katika safu ya ulinzi ya timu hiyo. Akiwa na umri wa miaka 34, Chiellini bado ana nguvu sana za kupambana uwanjani.

7. Thiago Silva (Paris Saint-Germain)


Siliva, 34 ni beki mwingine wa katikati, ambaye bado anaonekana kuwa imara akicheza mbele ya mkongwe mwenzake Buffon. Mbrazil huyo bado anaonekana kuwa bora licha ya kushuka kiwango msimu uliopita.


6. Jose Holebas (Watford)


Beki mwenye umri wa miaka 34 raia wa Ugiriki, bado ana kiwango cha kuridhisha. Mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa kufunga goli moja na ameshatoa 'assist' nne. Lakini katika michezo ya hivi karibuni ameonyesha kushuka kiwango kwa kiasi kikubwa sana.

5. Filipe Luis (Atletico Madrid)


Ni msimu mwingine na ni mwaka mwingine pia, lakini Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33 bado ni mtu muhimu sana katika safu ya ulinzi ya Atletico. Beki huyo ameisadia klabu hiyo inayoongozwa na Diego Simeone kuruhusu magoli manne pekee kwenye LaLiga msimu huu.

4. Sol Bamba (Cardiff City)


Akiwa na umri wa miaka 33, Bamba bado anajaribu kuisaidia Cardiff kupigana kurekebisha makosa yao. Uwezo wake wa kuruka juu unamsaidia kutawala wapinzani.


3. Pablo Zabaleta (West Ham)



Katika michezo mitano msimu huu, raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 ameonyesha kiwango cha kuridhisha, hasa kwenye mechi yao dhidi ya Manchester United.

2. Fernandinho (Manchester City),


Anaweza asifikie kiwango chake cha msimu uliopita, lakini Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33 bado ni mchezaji anayeaminika mbele ya Pep Guardiola.

1. Cristiano Ronaldo (Juventus)


Ingawa alikuwa na mwanzo mgumu katika suala zima la kufungai, Ronaldo, 33 amefanikiwa kufunga magoli 4 na kusaidia ufungaji wa magoli mengine manne kwenye Serie A tangu ajiunge na Juventus akitokea Real Madrid.

Orodha hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za WhoSocored.com, lakini haimanishi kwamba hao ndio wachezji pekee wenye umri mkubwa zaidi barani Ulaya.
Orodha ya wachezaji 11 wenye umri mkubwa zaidi barani Ulaya Orodha ya wachezaji 11 wenye umri mkubwa zaidi barani Ulaya Reviewed by Zero Degree on 10/18/2018 08:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.