Loading...

David de Gea 'alazimishwa' kusaini mkataba mpya United


Manchester United wametumia kifungu kwenye mkataba wa kipa wao David de Gea kinachowaruhusu kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.

Wamechukua hatua hiyo kuondoa utata kuhusu mustakabali wake, dirisha ndogo la kuhama wachezaji litakapofunguliwa Januari.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alijiunga na United kutoka Atletico Madrid mwaka 2011.

Mkataba wa sasa wa De Gea, 28, unafika kikomo mwisho wa msimu, jambo ambalo lingempa fursa ya kuanza kuzungumza na klabu nyingine kuanzia Januari 1 au hata kuingia kwenye mkataba wa awali.

Hata hivyo, United sasa wameamua kurefusha mkataba wake kwa mwaka mmoja.

Kama alivyothibitisha meneja Jose Mourinho baada ya ushindi wao wa Jumanne wa 1-0 dhidi ya Young Boys Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, United wanataka sana kusalia na kipa huyo.

De Gea ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa klabu United kwa miaka minne katika misimu mitano ambayo amekuwa nao.

Inaarifiwa kwamba De Gea yuko radhi kusalia klabu hiyo, lakini kufikia sasa bado hakuna makubaliano.

Wajume wake wanatilia maanani mshahara mkubwa ambao United walikubali kumlipa Alexis Sanchez alipojiunga nao kutoka Arsenal miezi 10 iliyopita.
David de Gea 'alazimishwa' kusaini mkataba mpya United David de Gea 'alazimishwa' kusaini mkataba mpya United Reviewed by Zero Degree on 11/30/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.