Gari la Jeshi lililokuwa limebeba Korosho kutoka Mtwara lapata ajali
Pichani gari lililopata ajali huku korosho zikiwa zimemwagika chini |
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo chanzo chake kilitokana na breki za gari hiyo kufeli, ambapo dereva na wengine waliokuwepo kwenye gari hilo wanaendelea vizuri.
"Gari hilo lilipata ajali jana jioni Novemba 21, chanzo chake ni kufeli breki kwa gari hilo la jeshi", amesema RC Byakanwa.
Hayo yanajiri baada ya Rais Dkt. John Magufuli kukabidhi rasmi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuzichukua korosho hizo baada ya kuzuia wafanyabishara kununua korosho kwa bei ya chini.
Rais alisema kuwa serikali iko tayari kununua korosho hizo kwa gharama ya shilingi 3,300 badala ya shilingi 3000 za kitanzania ambayo ni sawa na dola 1.4.
"Gari hilo lilipata ajali jana jioni Novemba 21, chanzo chake ni kufeli breki kwa gari hilo la jeshi", amesema RC Byakanwa.
Hayo yanajiri baada ya Rais Dkt. John Magufuli kukabidhi rasmi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuzichukua korosho hizo baada ya kuzuia wafanyabishara kununua korosho kwa bei ya chini.
Rais alisema kuwa serikali iko tayari kununua korosho hizo kwa gharama ya shilingi 3,300 badala ya shilingi 3000 za kitanzania ambayo ni sawa na dola 1.4.
Gari la Jeshi lililokuwa limebeba Korosho kutoka Mtwara lapata ajali
Reviewed by Zero Degree
on
11/22/2018 07:50:00 AM
Rating: