Loading...

Hakuna kitakachoharibika nikikosa Ballon d’Or - Luka Modric

Modric alishinda mpira wa dhahabu kwa kuibuka mchezaji bora kwenye Kombe la Dunia 2018
Nahodha wa timu ya taifa ya Croatia Luka Modric amesama kwamba hapoyezi muda wake kuiwaza Ballon d’Or. Modric pamoja na timu yake ya taifa walikubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Waingereza. Uingereza ilifuzu kwenda fainali ya Ligi ya Mataifa wakati Croatia ikishushwa chini.

Akizungumza baada ya Croatia kupoteza mchezo huo, Modric alielezea kauli yake ya kutokuwa na hofu ya tuzo ya Ballon d’Or. Kiungo huyo wa klabu ya Real Madrid alisema, “Mara ya mwisho nilisema kuwa najisikia kuheshimiwa kwa kuwa miongoni mwa wagombea wa tuzo kubwa kama hiyo. Kama ikitokea nikawa mshindi, hakuna atakayekuwa na furaha zaidi yangu, lakini kama sitapata tuzo hiyo, hakuna kitakachoharibika. Mwaka wangu ulikua mzuri na hivyo ndivyo ilivyo.”

Modric alishinda taji la UEFA mwezi Mei kisha akaiongoza Croatia hadi fainali ya Kombe la Dunia mwezi Julai
Mwaka 2018 umekuwa mzruri kwa Modric. Alishinda taji la Ligi ya Mabingwa mwezi Mei kabla ya kuiongoza Croatia hadi kufika hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mwezi Julai. Modric alifunga magoli mawili kwenye Kombe la Dunia na kushinda mpira wa dhahabu kwa kuibuka mchezaji bora wa michuano hiyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya na tuzo ya mchezaji bora wa FIFA. Hivyo, wengi wanamchukulia Modric kama mgombea anayetarajiwa kushinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or. Zimesalia wiki mbili tu, kujua ama atashinda tuzo hiyo au la.
Hakuna kitakachoharibika nikikosa Ballon d’Or - Luka Modric Hakuna kitakachoharibika nikikosa Ballon d’Or - Luka Modric Reviewed by Zero Degree on 11/20/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.