Iran yaapa kuendelea kuuza mafuta licha ya vikwazo ilivyoekewa
Rais wa Iran Hassan Rouhani |
Rais huyo ameuwambia mkutano wa kiuchumi uliotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni ya kitaifa kwamba Marekani ilitaka kuzuwia mauzo ya mafuta ya Iran, lakini wataendelea kuuza mafuta hayo licha ya vikwazo walivyoekewa.
"Tumekuwa tukiuza mafuta yetu na tutaendelea kuyauza katika hali yoyote ile. Tuna haki ya kufanya hivyo. Wansema iran inakiuka vikwazo ndio tunasema wazi kwamba tutakiuka vikwazo vyenu ambavyo havifai ni vya uonevu na vinavyokandamiza na vipo kinyume cha kanuni za kimataifa. Marekani itajuta. Tutarejesha uwekezaji wa kigeni humu nchini," alisema Hassan Rouhani.

Ijumaa iliopita Marekani ilisema itaruhusu kwa muda mataifa manane yanayoagiza mafuta ya Iran kuendelea kununua mafuta hayo wakati itakapoiekea tena vikwazo Iran hii leo, vinavyonuiwa kuishinikiza nchi hiyo kuachana na mpango wake wa nyuklia, makombora na shughuli zake za kikanda.
China, India, Korea Kusini, Japan na Uturuki, mataifa makubwa yanayoagiza mafuta kutoka Iran, ni miongoni mwa nchi hizo nane zinazotarajiwa kuendelea kununua mafuta ya taifa hilo la kiislamu ili kuhakikisha bei ya mafuta ghafi haiyumbi.
Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Iran Bahram Qasemi, nchi yake bado inamawasiliano na mataifa mengine yaliotia saini mkataba wa nyuklia mwaka 2015. Amesema kwa sasa wanamikakati ya kuendelea na biashara na Umoja wa Ulaya, Qasemi ameongeza kuwa japo suala hilo linaonekana kuchukua muda lakini tayari wameanza kulifanyia kazi.

Source: DW
Iran yaapa kuendelea kuuza mafuta licha ya vikwazo ilivyoekewa
Reviewed by Zero Degree
on
11/05/2018 01:18:00 PM
Rating: