Loading...

KRC Genk ya Samatta yang’ang’aniwa Ubelgiji


KIKOSI cha KRC Genk anachokichezea mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, kimelazimishwa sare ya bao 1-1 na Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, uliochezwa Uwanja wa Luminuz Arena nchini Ubelgiji.

Katika mchezo huo, Samatta alicheza kwa dakika zote 90.

Genk iliandika bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Dieumerci N’Dongala, lakini Siebe Schrijvers aliisawazishia Brugge dakika ya 53.

Sammata sasa amefikisha michezo 127 katika mashindano yote tangu alipojiunga na Genk, Januari mwaka 2016, akitokea TP Mazembe ya DRC.

Akiwa na Genk, Samatta tayari amefunga jumla ya mabao 51.

Katika ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 99 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane, mabao mawili na Europa League mechi 20, mabao 14.
Genk inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imejikusanyia pointi 34 baada ya sare ya jana dhidi ya Brugge.
KRC Genk ya Samatta yang’ang’aniwa Ubelgiji KRC Genk ya Samatta yang’ang’aniwa Ubelgiji Reviewed by Zero Degree on 11/05/2018 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.