Loading...

Makambo aja na kali nyingine Yanga


Baada ya kufunga bao kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC, juzi, mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo raia wa DR Congo amesema sasa watapambana kuhakikisha wanapata ushindi kila mechi inayofuata.

“Kazi yangu ninapokuwa Yanga ni kucheza na kufunga hivyo kama kocha atanipa nafasi nitajituma zaidi ili timu yangu iweze kupata matokeo katika kila mchezo ambao tunacheza.

"Uliona Mwadui walivyokuwa wakicheza vizuri na sisi tuliliona hilo na tukajituma na tukapata ushindi, tutafanya hivyo kila mechi.

“Kama kocha atanipanga katika mchezo ujao nitajituma kadiri niwezavyo ili nifunge na timu yangu iweze kupata pointi tatu muhimu,” alisema Makambo mwenye mabao matano.

Chanzo: SaleJembe
Makambo aja na kali nyingine Yanga Makambo aja na kali nyingine Yanga Reviewed by Zero Degree on 11/25/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.