Mifuko ya plastiki kuzidi samaki baharini
Kwa sasa kila Mtanzania anakadiriwa kutumia mifuko mitatu hadi minne kwa wiki, huku ikielezwa kuwa kwa mwaka Tanzania inatumia mifuko bilioni nane hadi 10 na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti mifuko hiyo, inakadiriwa kwamba ifikapo 2050 takataka za plastiki zitakuwa nyingi baharini kuliko samaki.
Pia imeeleza kuwa kutokana na baadhi ya nchi jirani kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki na kuruhusu uzalishaji kwa ajili ya soko la nje ya nchi, pamekuwepo na wimbi kubwa la uingizaji wa mifuko ya plastiki nchini ikiwemo kupitia njia zisizo rasmi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau kuhusu fursa ya uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine alitoa angalizo kuwa ni muhimu bei ya mifuko mbadala ikawa nafuu na kwa kiwango ambacho wananchi wengi wanamudu.
Balozi Sokoine alisema vifungashio vya plastiki huchukua muda mrefu kuoza katika mazingira takriban miaka 500 hadi 1,000 na kwa maneno mengine huchukua karne kadhaa kuoza katika mazingira.
Alisema bidhaa za plastiki zilianza kutumika kwa wingi duniani kote katika miaka ya 1950 na zina matumizi mengi ikiwemo vifungashio vya vyakula, dawa na mbolea, samani za majumbani kama viti na meza, vifaa vya ujenzi kama vile mabomba ya maji na hata mavazi.
Alisema zaidi ya nusu ya bidhaa hizo hutumika kama vifungashio au mifuko ya kubebea bidhaa, ambako sehemu kubwa huishia baharini ambapo kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, zaidi ya asilimia 80 ya takataka zilizopo baharini hutokea nchi kavu.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa takriban nusu ya taka za plastiki zinazozalishwa zinajumuisha vifungashio na mifuko ya plastiki na uwezo wa usimamizi na udhibiti wa taka za plastiki ni hafifu.
Alisema suala hilo si tu ni hatari kwa afya ya jamii na hifadhi ya mazingira, bali linagusa uchumi na mustakabali wa maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo. Aidha, alisema kwa kuwa mifuko hiyo huelea katika maji kwa muda mrefu huchangia katika kusafirisha vimelea vya magonjwa kutoka eneo moja hadi jingine.
Alisema changamoto ya udhibiti wa vifungashio na mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa ni suala la dunia nzima inayohitaji hatua za haraka hivyo ni muhimu kama Taifa likashirikiana na jumuiya ya kimataifa kwa kuchukua hatua madhubuti ili kuinusuru dunia dhidi ya janga hilo.
Alisema kikao hicho kimelenga kupata mwelekeo wa kuchukua hatua muafaka ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaochangiwa na mifuko ya plastiki ikiwemo kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya mifuko mbadala iliyo rafiki kwa mazingira ikiwemo ya karatasi, vitambaa vya nguo na hata vikapu vya asili.
Alisema uwekezaji katika mifuko mbadala ni fursa maridhawa kutokana na uwepo wa teknolojia zenye gharama nafuu na rahisi kwa mazingira ya nchi ya kiuchumi na kijamii.
Naye Mhandisi Viwanda, Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Enock alisema mkutano huo unajumuisha wamiliki wa viwanda vinavyozalisha bidhaa za karatasi, wawakilishi wa sekta binafsi, baadhi ya wizara na taasisi za serikali.
Alisema changamoto za usimamizi wa taka za plastiki ni nchi kugeuzwa dampo la mifuko ya plastiki, kwani zipo nchi zimezuia bidhaa hizo ila zimeruhusu viwanda vyao kuzitengeneza na kuziuza nje ya nchi zao ikiwemo Tanzania.

Ofisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar, Haidar Bakari Machano alisema wanaendelea na udhibiti wa mifuko hiyo ambapo kuanzia Oktoba 2011 hadi Julai 2018, jumla ya tani 7.6 za mifuko ya plastiki na wafanyabiashara 548 wamekamatwa.
Mifuko ya plastiki kuzidi samaki baharini
Reviewed by Zero Degree
on
11/08/2018 08:35:00 AM
Rating: