Loading...

Msiba wageuka kuwa sherehe baada ya marehemu kufufuka

Msiba wageuka kuwa sherehe(Picha: SIBU SIRE COMMUNICATION)
Wanakijiji wa kijiji kimoja nchini Ethiopia washeherekea kufufuka kwa mwanaume mmoja ambaye alidhaniwa kuwa amekufa.

Hirpha Negero, ambaye ni baba wa watoto watano alitangazwa kuwa amefariki siku ya jumanne ,majira ya saa nne na nusu.

Kulingana tamaduni zao katika vijiji vya pembezoni mwa miji vilivyopo Sibu Sire na mkoa wa Oromia,bunduki ilipigwa mara mbili na hiyo ni ishara kuwa kuna mtu amefariki hivyo watu wanaitwa kuhudhuria katika msiba.

Ndani ya saa moja, mwanakijiji mmoja kwa jina la Etana Kena alimuweka kwenye jeneza tayari kwa mazishi.

Ingawa wakati wa mazishi katika majira ya saa tisa na nusu, walisikia mtu akigonga kutoka katika jeneza.

''Watu walishangaa na huku wengine wakikimbia na hata sikupata mtu wa kunisaidia," bwana Etana alieleza namna alivyohitaji msaada ili aweze kulifungua jeneza.said.

Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, mtu huyo aliyefufuka alisema: "Nilisikia sauti ya mtu akilia. Nlikuwa sina nguvu kabisa n ahata sikuweza kuongea."

Lakini badaye aliweza kuanza kuita.

Baada ya mshtuko ambao uliwapata wengi katika msiba, mazishi yaligeuka kuwa sherehe.
Msiba wageuka kuwa sherehe baada ya marehemu kufufuka Msiba wageuka kuwa sherehe baada ya marehemu kufufuka Reviewed by Zero Degree on 11/25/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.