Loading...

Mwijage aanza kuwapigania wananchi wake bungeni


Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage ameitaka Serikali kuharakisha inapeleka umeme katika jimbo lake ili wananchi wanufaike na miradi ya umeme vijijini (Rea).

Mwijage ambaye alivuliwa nafasi ya uwaziri wa viwanda, biashara na uwekezaji wiki iliyopita, kabla ya kuuliza swali bungeni leo, alimshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na uongozi wa Bunge kwa namna walivyompa ushirikiano wakati wote wa utendaji kazi na viongozi wa dini wanaomuombea wakati wote. 

Mbunge huyo huku akishangiliwa, alisema wananchi wake walipata mradi wa umeme katika jimbo zima lakini maeneo mengi yaliishia kuwekwa mambo bila ya kusimikwa kwa nguzo.

"Ni lini sasa Serikali itawaondolea kero ya umeme ili wananchi wale nao waanze kunufaika na miradi ya Rea," alisema Mwijage

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema miradi ya umeme katika wilaya ya Muleba itatekelezwamuda si mrefu na mkandarasi yuko katika maandalizi ya kupeleka nguzo.
Mwijage aanza kuwapigania wananchi wake bungeni Mwijage aanza kuwapigania wananchi wake bungeni Reviewed by Zero Degree on 11/16/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.