Ngorongoro Heroes yachapwa 2-0 na Burundi michuano ya AFCON
Mchezo huo uliofanyika mjini Bujumbura, Ngorongoro Heroes imepoteza kwa mabao 2-0 na kuanza vibaya katika harakati za kufuzu michuano hiyo itakayofanyika nchini Misri mwaka 2019.
Mabao ya Burundi yamefungwa katika kipindi cha pili kupitia kwa Shaban Mabano aliyeanza kuipatia timu yake bao katika dakika ya 59 kabla ya Cedric Mavugo kufunga bao la pili katika dakika ya 79.
Baaya ya mchezo huo, Ngorongoro Heroes inatarajia kurejea nyumbani kwaajili ya maandalizi kwaajili ya mchezo wa marudio ambao utachezwa wiki ijayo.
Ngorongoro Heroes inahitaji kushinda mchezo wa marudio hapa nchini kwa idadi ya mabao matatu au zaidi. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, wachezaji wanaotakiwa kushiriki ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 1997.
Pia mechi hizo za kufuzu michuano ya AFCON U-23, zitatumika kwaajili ya kuwapata wawakilishi wa Afrika katika mashindano ya Olympic yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020.

Reviewed by Zero Degree
on
11/14/2018 07:05:00 PM
Rating: