Loading...

Yaliyojiri baada ya Wambura kutinga TFF kibabae


MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, jana alitinga katika ofisi za shirikisho hilo kibabe baada ya kukaa nje kwa takribani miezi tisa tangu alivyofungiwa mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Wambura maisha kutojihusisha na soka kutokana na kukutwa na makosa matatu, ikiwemo kuchukua fedha za TFF ambazo ni malipo yasiyokuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Pili, kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo siyo halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013. Na Tatu, ni kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015. Akizungumza na Championi Jumatano, Wambura alisema:

“Nimefikisha shauri la Mahakama Kuu juu ya kutengua maamuzi ya Kamati ya Maadili ya TFF ambayo ilinifungia maisha iliyotolewa tangu Novemba 30, mwaka huu, mimi ni makamu wa rais wa TFF, nimeleta ili wasije kusema hawakupata taarifa.

“Imekuwa ikizungumzwa kuhusu kupeleka masuala ya mpira mahakamani, kilichokwenda kuzungumzwa ni suala la uvunjifu wa sheria uliofanywa na Kamati ya Maadili ya TFF na si kupeleka masuala ya mpira mahakamani, kabla sijalipeleka shauri hili mahakama kuu, niliwaandikia barua TFF tarehe 16 mwezi wa nne kuomba kulimaliza suala hilo kabla ya kufika huko, walikaa kimya.

“Wanachotakiwa kufanya TFF ni kufuata njia mbili aidha kukubaliana na maamuzi ya mahakama ama kukata rufaa na iwapo watakaa kimya watakuwa wamedharau mahakama na itakuwa chombo cha kwanza kuidharau mahakama.

Wasipotekeleza basi njia bora itakuwa kulipeleka suala hili FIFA. “Natarajia kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe ambaye ndiye msimamizi wa michezo nchini ili tuweze kumueleza na aweze kutusaidia kwa upande wa serikali.”
Yaliyojiri baada ya Wambura kutinga TFF kibabae Yaliyojiri baada ya Wambura kutinga TFF kibabae Reviewed by Zero Degree on 12/05/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.